Saturday 7 December 2013

HII NDIYO RATIBA YA MAZISHI YA NELSON MANDELA, WATANZANIA WAPEWA NAFASI YA KUHUDHURIA SIKU 5 ZA MAMBOLEZO ZATANGAZWA!

 
 
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma ametangaza mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 mwaka huu kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini.
 
Rais Zuma ametangaza siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinton na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.
 
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
 
Mwili wake utawekwa katika jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi.
Hata hivyo watanzania mbalimbali waishio nchini humo wamepewa nafasi ya kushiiki kwenye mazishi hayo.

No comments: