Saturday 7 December 2013

KOCHA WA SIMBA MIEZI SITA ATAIBADILI SIMBA YA KIBADEN?


SARAKASI za uongozi ndani ya klabu ya Simba bado zinaendelea huku pande mbili zinazolumbana kushika hatamu ya uongozi, kila upande ukimtangaza kocha wake.

Upande wa kwanza unaongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ umempa kazi Kocha raia wa Croatia, Zdravko Logarusic wakati upande wa pili unaoongozwa na Mwenyekiti Ismail Aden Rage, ukisema bado Abdallah Kibadeni ndiye kocha.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo, upande wa Mzee Kinesi ndiyo unaoonekana umeshinda kwani tayari Logarusic ameshatua nchini na ameshaanza kazi ya kuifundisha Simba kwenye mazoezi yake yanayoendelea kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar es Salaam.

Ina maana kwamba kambi ya Mzee Kinesi ndiyo inayomilikia timu kwa sasa na timu ndiyo Simba yenyewe. Upande mwingine unaweza kuwa unamiliki majengo ya kufanyia mikutano lakini hatamu ya timu ipo mikononi mwa kundi linalompinga Rage




Simba imeingia mkataba wa miezi sita na Logarusic ili ainoe klabu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara lakini nyuma ya pazia kuna mambo mengi nyuma yake.

Kwanza Logarusic anakutana na kikosi ambacho hamfahamu mchezaji hata mmoja wa Simba, kidogo ingekuwa rahisi kwake kama angalau angekuwa na ufahamu hata mdogo wa kikosi cha timu hiyo.

Hii inamaanisha kwamba, Logarusic sasa anaenda kukibomoa kikosi cha kwanza cha Simba ambacho kwa kiasi fulani kilikuwa kimeshaanza kuaminiwa na Kibadeni.

Sasa Logarusic anawasubiri wachezaji wa Simba waliopo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars na Zanzibar Herose ambao wapo Nairobi Kenya wakishiriki fainali za Kombe la Chalenji zinazofikia tamati Desemba 13 mwaka huu.

Kwa kuwa Logarusic hana cha kupoteza ndani ya miezi sita yake ya mkataba moja kwa moja hawezi kuwa na mawazo ya mbali zaidi katika kuifundisha klabu hiyo kwani, anafahamu fika hata afanyeje hali inaweza kuwa tofauti kwake baada ya muda huo.

Tazama hata usajili uliofanywa na Simba haujulikani kama umefuata ripoti ya nani kati ya kamati ya utendaji na ile ya Kibadeni ambayo inaelezwa haina mambo mengi ya kiufundi.



Nipo na George Masatu...

No comments: