Wednesday 11 December 2013

Makamu wa marais na mawaziri waapishwa Sudan

Rais Omar al-Bashir amehudhuria sherehe za kuapishwa kwa makamu wa marais wawili walioteuliwa hivi karibuni pamoja na wasaidizi na mawaziri wapya, ambao wote wanatoka Chama tawala cha National Congress CNP. Mabadiliko ya baraza la mawaziri nchini Sudan yamekuja baada ya nchi hiyo kuendelea kukumbwa na hali ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa. Makundi ya waasi wa Sudan ambao mara kwa mara wanalalamikia hali ya kuwekwa kando na maendeleo yasiyo na uwiano katika maeneo nje ya Khartoum, wanaendelea na mapambano, huku hali ya kuzorota kwa uchumi mjini Khartoum na kupanda kwa bei za bidhaa zikisababisha malalamiko na vifo vya watu wengi katika mwezi Septemba mwaka huu.

No comments: