Wednesday 11 December 2013

Umoja wa Mataifa wapeleka ndege za Drone Congo.

Umoja wa Mataifa utaanza kurusha ndege zenye kamera zisizotumia rubani-Drones - kwenye anga ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC hapo Jumanne  ili kuwasaidia walinda amani kuwasaka waasi na kufuatilia mienendo yao.

Mkuu wa walinda amani katika Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous yupo mjini Goma kushuhudia uzinduzi huo wa Drones. Alisema Jumatatu kwamba hali huko mashariki mwa Congo ni tofauti sana kutoka mwaka mmoja uliopita wakati kundi la waasi wa M23 walipoiteka miji kadhaa katika eneo hilo.

Mwezi uliopita kundi la M23 lilitangaza kuweka chini silaha zake baada ya jeshi la Congo kuteka ngome ya mwisho ya kundi hilo kwa msaada wa kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa.

No comments: