Sunday 8 December 2013

Yadaiwa Kim Jong Un ameuwa wasaidizi wake

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Shirika la upelelezi la Korea Kusini limesema linaamini kuwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un amemfukuza kazi mjomba wake kutoka  nafasi ya juu ya jeshi na kuwauwa baadhi ya wasaidizi wake.

Wabunge walielezwa na shirika la taifa la kijajusi la Seoul Jumanne kwamba mjombake kiongozi huyo, Jang Song Thaek alifukuzwa kazi kama  makamu mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ulinzi yenye nguvu.

Wabunge  hao walisema shirika hilo linaamini kwamba wafanyakazi wa wawili wa karibu wa Jang,  Leeyong–ha na Jang Soo–Keel waliuwawa mwezi Novemba na  kwamba mjombake kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, hajaonekana tangu wakati huo.

No comments: