Tuesday 10 December 2013

Yanayojiri kwenye misa ya wafu ya Mandela


Maelfu wamekaidi hali mbaya ya hewa na kufurika uwanja wa FNB kuhudhuria misa ya wafu ya rais mstaafu wa Afrika Nelson Mandela. Je una ujumbe wowote kwa watu wa Afrika Kusini?

. Je uko Afrika Kusini? nini kinajiri huko mbali na misa hii kufanyika?

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aanza kuwahutubia wananchi waliofika kwa misa ya wafu ya Mandela



 Obama: ''Hatutawahi kuwa na kiongozi kama Mandela duniani tena. Lakini nataka kuwashauri vijana kote Afrika na duniani kote kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo zake Mandela.''

 Obama :'Kumbukumbu za Mandela hunifanya kila siku kutaka kuwa mtu mwema na nataka kuwashauri vijana kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo za Mandela'
 Obama: ''Asanteni sana kwa kuturuhusu kumuenzi Nelson Mandela, alikuwa mkombozi aliyetetea demokrasia na anaweza tu kufananishwa na marehemu Mahatma Ghandi. Ni vyema kumkumbuka Mandela kama mtu aliyejitolea sana na hakuogopa kushauriana nasi kuhusu maoni yake na hisia zake na kwa sababu Mandela aliweza kukubali kuwa mtu wa kawaida mtu ambaye aliweza kufanya makosa kama mwanadamu mwengine yeyote ule.''
Barack Obama kwenye misa ya wafu ya Mandela
.Rais wa Marekani Barack Obama aanza kuhutubia wanachi wa Afrika Kusini wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela
.Dlamini Zuma, 'Tunamuenzi Madiba, alikuwa shujaa aliyekuwa tayari kusikiliza maoni ya watu wengine licha ya kukinzana na yake. Ni shujaa wa Afrika ambaye alijitolea kuikiomboa Afrika na juhudi hizo hazikuwahi kumuondoka daima hadi kifo chake.''
 am Mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika Dr Nkosazana Dlamini Zuma anahudhuria umati wa watri kwenye misa hiyo


 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemaliza kuhutubia umati wa watu waliokusanyika kwenye misa ya wafu ya Mandela

Ban Ki moon akihutubia watu uwanjan FNB
11:03 am Ban Ki Moon: ''Ni Muhimu sote kuendeleza sera za shujaa wetu Mandela''
11:00 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anahutubia umati wa watu waliokusanyika katika uwanja wa FNB

No comments: