Sunday 19 January 2014

RVP asema Moyes ndio kocha sahihi wa Man u

Kocha Moyes akizungumza jambo uwanjani na Robin Van Persie .Picha na Maktaba




Robin Van Persie, anaamini kwamba mtu yeyote anayeishabikia Manchester United ni lazima awe mvumilivu na kumruhusu Moyes kuweka mambo sawa klabuni baada ya kuanza kwa mguu mbaya.

KILA mtu hataki kumwamini moja kwa moja kocha wa Manchester United, David Moyes. Lakini mtu mmoja muhimu ndani ya Old Trafford amejitokeza na kudai kwamba kocha huyo ni mtu sahihi kabisa kuiongoza timu hiyo ya Old Trafford wakati huu.

Robin Van Persie, anaamini kwamba mtu yeyote anayeishabikia Manchester United ni lazima awe mvumilivu na kumruhusu Moyes kuweka mambo sawa klabuni baada ya kuanza kwa mguu mbaya.

Wababe hao wanashika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu England huku wakisuasua katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao na tayari imeshatolewa michuano ya FA.

“Nadhani anahitaji kupewa muda kama mtu mwingine yeyote, sana sana ukiwa mpya katika klabu kubwa kama hii. Kusema kweli sidhani kama watu hawaelewi kwamba inabidi wampe muda kidogo, hapa naongelea kuhusu mashabiki na hata sisi,” alisema staa huyo Mdachi.

Van Persie ambaye atalikosa pambano la kesho Jumapili dhidi ya Chelsea, alimzungizia Wayne Rooney ambaye kwa sasa yupo fiti baada ya jana Ijumaa kufanya mazoezi kivyake, huku kikosi hicho cha Moyes kikipata nguvu mpya kutokana na viungo Phil Jones na Marouane Fellaini kushiriki mazoezi na wenzao.

Mastaa hao watatu walikuwa majeruhi, lakini wanatajwa kuwa fiti kwa ajili ya kuivaa Chelsea baada ya kufanya mazoezi, ambapo Jones na Fellaini walikuwa fiti zaidi kwa muda wote wa mazoezi.

Kuhusu Rooney, Van Persie alisema: “Tunafahamu kuwa tunakuwa na nguvu sana tukicheza pamoja. Ukiwa na mchezaji wa kariba ya Wayne tunaweza kusonga mbele zaidi na zaidi. Mechi hii atafunga mawili, mechi ijayo nitafunga mawili. Ni muhimu kwamba kombinesheni inazidi kuwa imara.”

“Wote tunaweza kucheza mbele na tunaweza kushuka, huo ni ubora wa ziada ambao tunao. Ni kitu nadra sana. ukiangalia kuna washambuliaji wakuu, wafungaji, wawindaji katika boksi na namba 10 ambao wanashuka sana.”

“Mimi na Wayne wote wawili tunaweza kufanya kazi hiyo ingawa Wayne anafanya zaidi kidogo kwa sababu anacheza nyuma yangu, lakini wote tunaweza kuifanya kazi hiyo.”

No comments: