Monday 27 January 2014

Mwombeki aitia Simba aibu

KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic amesema aliamua kumtoa straika Betram Mwombeki dakika 20 baada ya kumuingiza dhidi ya Rhino Rangers ili kumsitiri kwa aibu ambayo angeipata kutoka kwa mashabiki.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Logarusic alimuingiza Mwombeki dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe.

Dakika chache baada ya kuingia uwanjani, Mwombeki alipoteza pasi tatu ndani ya dakika nane hali iliyomfanya Logarusic ampigie kelele za kuelekeza kila anapokosea.

Mara kadhaa Mwombeki alipokuwa akikosea alionekana kujutia kosa lake kwa kujaribu kukaba ili apokonye mpira aliopoteza, lakini Logarusic alikuwa akishika kichwa kuonyesha kutopendezwa na makosa hayo. Uvumilivu ulimshinda kocha huyo kwani dakika 85 alimtoa Mwombeki na kumuingiza Henry Joseph. Wakati anatoka straika huyo alisalimiana na Logarusic ikiwa ni ishara ya kutokuwepo kwa tatizo baina yao.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Logarusic alisema alilazimika kumtoa Mwombeki kutokana na kushindwa kutimiza alichotumwa uwanjani akitokea benchi pia kumsitiri kwa aibu ya kuzomewa na mashabiki.

“(Mwombeki) alikuwepo benchi kuona makosa ya wenzake, lakini alipoingia kila mtu ameona alichokuwa anafanya, mashabiki wakaanza kumpigia kelele ndipo nikaona nimsitiri kwa kumtoa maana angebaki angepata aibu zaidi,”

No comments: