Friday 24 January 2014

Serikali yatoa masharti kwa Chama cha Muslim Brotherhood

Hazem Beblawi

Waziri Mkuu wa Mpito wa Misri ameambia BBC kuwa wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood wanaweza kushiriki Uchaguzi Mkuu ikiwa watalaani ghasia na machafuko.

Hazem Beblawi alisema kuwa kura ya maoni ya mwezi uliopita kuhusu Katiba mpya ilikuwa hatua ya kwanza kurejesha demokrasia na kuwa itafuatwa na Uchaguzi wa urais na ubunge katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Lakini vugu vugu la Muslim Brotherhood, ambalo liliorodheshwa kuwa kundi la kigaidi hivi karibuni, limekanusha madai ya kuhusika na ghasia zinazokumba Misri.

Chama hicho cha Muslim Brotherhood, kiliongoza serikali ya kwanza kuwahi kuchaguziliwa kwa njia ya demokrasia nchini Misri, ambayo iliondolewa madarakani miezi sita iliyopita na jeshi.

Kiongozi wake Mohammed Morsi anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya kihalifu.

No comments: