Thursday 30 January 2014

Tambwe akata tamaa kuwa mfungaji bora

Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amesema itamwia vigumu kuibuka kinara wa upachikaji mabao kama waamuzi wataendelea kuchezesha vibaya kwenye Ligi Kuu Bara.

Tambwe alisema hayo baada ya mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani kukataa mabao yake mawili kwa madai alifanya makosa kabla ya kufunga.

Mshambuliaji huyo raia wa Burundi alifunga mabao hayo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Rhino Rangers uliopigwa mwishoni wiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Tambwe alisema mwamuzi Shamba hakuwa sahihi kukataa mabao yake kwa sababu hayakuwa na matatizo yoyote.

“Binafsi naamini mabao niliyofunga yalikuwa halali kabisa ingawa mwamuzi alikataa, sisemi kama aliwapendelea wapinzani, lakini inawezekana hana uwezo.

“Hofu niliyonayo ni kama waamuzi wa aina hii wataendelea kupewa nafasi ya kuchezesha itakuwa vigumu kwangu kutimiza malengo yangu ya kumaliza ligi nikiwa mfungaji bora,”alisema Tambwe.

No comments: