Monday 14 April 2014

Jezi za Ronaldo zaongoza kwa mauzo

Jumla ya jezi milioni 1 za mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ziliuzwa msimu wa mwaka 2013/14 na kuzidi jezi za timu nzima ya Bayern Munich ambayo iliuza jezi 880,000.

Ronaldo hivi sasa ndiye anayeshikilia tuzo ya mchezaji bora duniani, pia bidhaa mbalimbali zenye jina lake zinanunulika sana sehemu mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani, klabu za Real Madrid na Manchester United ndiyo zilizoongoza baada ya kila moja kuuza jezi 1.4 milioni mwaka 2013, lakini kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu mauzo ya Manchester United yaliongezeka.

Mwaka huu jezi za wachezaji wa Real Madrid kila moja inauzwa Dola 76 za Kimarekani wakati mwaka jana zilikuwa zikiuzwa Dola 84 za Kimarekani (Dola 1= Sh1,620).

Gazeti hilo pia lilitaja wachezaji ambao wameziwezesha klabu zao kuuza jezi nyingi kuwa ni Real Madrid (Ronaldo, Bale, Xabi, Alonso), Man United (Rooney, van Persie, Mata), Barca (Messi, Neymar, Xavi), Chelsea (Hazard, Oscar, Lampard), Bayern (Ribery, Lahm, Schweinsteiger, Liverpool (Suarez, Coutinho, Sturridge), Arsenal (Ozil, Wilshere, Ramsey), Juventus (Pirlo, Pogba, Tevez), Inter Milan (Zanetti, Palacio, Nagatomo), AC Milan (Kaka na Mario Balotelli).

No comments: