Wednesday 16 April 2014

Rais wa Burundi tena kugombea muhula watatu

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza bungeni, mjini Paris, nchini Ufaransa, machi 12 mwaka 2013.Upinzani nchini Burundi umedhani utafanya vizuri katika chaguzi zijazo za mwaka 2015, baada ya bunge kutoidhinisha rasimu ya marekebisho ya katiba, ambayo ingelimpa nafasi rais wa Burundi Peirre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu, baada ya kugombea mihula miwili (2005-2010 na 2010-2015).

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana, bunge kutoidhinisha rasimu ya marekebisho ya katiba haimkatazi rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa mara nyingine tena kiti cha urais katika chaguzi za mwaka 2015.
Ni kwa mara ya kwanza waziri Edouard Nduwimana anatangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine kwa rais Nkurunziza kwenye kiti cha urais.
Waziri Edouard Nduwimana ameyasema hayo katika kikao na viongozi wa dini.
Tanzgazo hilo la waziri Nduwimana limezua tafrani na utata baina ya wanasiasa na vyama vya kiraia nchini Burundi.
“Haya ninaya, kutokana na kwamba kuna watu ambao wamekua wakikifikiria kwamba rais Nkurunziza hawezi kugombea muhula mwengine, si kweli.
Ninawasihi wanasiasa ambao watagombea kwenye kiti cha urais, wajiandae wakijua kwamba watagombea kwenye nafasi hio pamoja na rais alie madarakani sasa.
Korti ya katiba ndio itaamua, na raia ni lazima waheshimu uamzi utakao kuwa umetolewa na korti ya katiba”, amesema Edouard Nduwimana.
Edouard Nuwimana ni kutoka chama tawala CNDD-FDD, na ni mmoja kati washirika wa karibu wa rais Pierre Nkurunziza.
Chama cha CNDD-FDD, kupitia msemaji wake Onesime Nduwimana, kimesema bado hakijakutana ili kiamuwe atakayegombea kwa tiketi yake kwenye kiti cha urais katika chaguzi za 2015.
Muungano wa vyama vya upinzani ADC-Ikibiri, kupitia msemaji wake, Chauvineau Mugwenezo, kimebaini kwamba kauli ya waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana, imekua kila mara ikitafsiri nia ya rais Nkurunziza.
Chauvineau Mugwengezo ambaini kwamba jambo hilo la rais Nkurunziza kugombea muhula mwengine halitawezekana.
Vyama vya kiraia vimegawanyika kufuatia tangazo la waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana.
Kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia kwa ajili ya maendeleo (Focode), Acifique Ninahazwe, amesema iwapo rais Nkurunziza atagombea muhula wa tatu, atakua amekiuka katiba ya nchi na mkataba uliyoafikiwa na raia wa Burundi kutoka tabaka mbalimbali mjini Arusha nchini Tanzania mwaka wa 2000.
Kwa upande wake, Samuel Nkengurukiyimana, kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia (PISC-Burundi), amesema kwamba waziri wa mambo wa ndani si msemaji wa rais Nkurunziza, huku akibaini kwamba rais Nkurunziza hajafanya mihula miwili, bali ni muhula umoja, ambao ni toka mwaka 2010 hadi 2015.
“ Kuwa madarakani kwa rais Nkurunziza toka mwaka 2005 hadi 2010, si muhula, kama jinsi baadhi wanafikiri, kwani wakati huo rais hakua na uwezo wa kufuta bunge, licha ya kuwa alichaguliwa na wabunge, ambao pia walichaguliwa na raia”, amesema Nkengurukiyimana.
Hivi karibuni muakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu, Russ Feingold, amewataka marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Rwanda kuheshimu katiba za nchi zao, hasa kuheshimu ibara zinazopiga marufuku marais kugombea mihula iliyo juu ya idadi iliyopangwa.

No comments: