Wednesday 16 April 2014

Serikali ya Burundi yakanusha tuhuma ya usambazaji wa silaha

Serikali ya Burundi imeelezea jana kughadhabishwa kwake uvumi uliosambazwa kuwa imejishughulisha na usambazaji wa silaha kwa wanamgambo wa chama tawala cha CNDD -FDD na kuiomba ofisi ya Umoja wa mataifa nchini humo kuomba radhi kutokana na matamshi yake.

Siku za hivi karibuni, vyombo vya habari nchini Burundi vimeweka wazi waraka wa ndani wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo ambao umezungumzia usambazaji wa silaha mwezi Januari kwa vijana na wanachama wa chama tawala” Imbonerakure”.
Katika mkutano na mabalozi wakiwemo waandishi wa habari jana mjini Bujumbura makamu wa kwanza wa rais, Prosper Bazombaza ametupilia mbali tuhuma hizo na kusema kuwa madai hayo ni uvumi ulioibuka kama mbinu ya uchaguzi mkuu unaokaribia.
Hivi Karibuni Umoja wa Mataifa ulitoa onyo kali kwa Serikali ya Burundi na kuitaka kuchukua hatua za haraka kushughulikia vurugu za kisiasa na kuheshimu haki za binadamu.
“Tuna imani kwamba serikali ya Burundi itazingatia haraka iwezekanavyo na kushughulikia (matatizo yote) yanayosababisha vurugu na ukiukwaji wa haki za bin adamu”, alisema msemaji wa Umoja wa Matiafa Stéphane Dujarric.
Aidha, umoja huo ulibainisha kuwa endapo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na uchochezi wa vurugu vitaendelea, basi wahusika watawajibika mbele ya mahakama za kimataifa.
Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kitengo cha kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng alifanya ziara mjini Bujumbura juma liliyopita, ambako alijadili hofu hio ya kutokea kwa mauaji ya kimbari na viongozi wa Burundi .
Onyo hilo ni miongoni mwa tahadhari ziliyokua zikitolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa pamoja na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akiwa pamoja na rais Pierre Nkurunziza  juni 9 wakati wa ziara yake mjini Bujumbura.
Akiwa ziarani mjini Bujumbura hivi karibuni, balozi Samantha Power, aliwatajka viogozi wa Burundi kuheshimu uhuru wa kisiasa, na vilevile kuheshimu katiba ya nchi, ambayo utawala unajaribu kuifanyiya marekebisho.
“ Tunasisitiza kuheshimu katiba ya nchi, ambayo ni sheria mama ya Burundi, na vilevile kuheshimu haki za binadamu,” alisema Samantha Power baada ya mazungumzo na rais Pierre Nkurunziza.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilielezea aprili mosi wasiwasi wake, juu ya mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.
Katika tangazo liliyotolewa alhamisi aprili 10 mwaka 2014, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilielezea kwa mara nyingine wasiwasi wake juu ya uhuru wa kujieleza na mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa vya upinzani na mashirika ya kiraia.
Wajumbe 15 wa baraza hilo, walielezea juma liliyopitas wasiwasi wao juu “ya vitisho na kufungwa kiholela pamoja na machafuko yanayotekelezwa na vijana kutoka vyama vya kisiasa”.
Wajumbe hao walitoa wito kwa serikali ya Burundi kutowafumbia macho wafuasi wa chama tawala ambao wamekua wakijihusisha na maovu mbalimbali, mkiwemo unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa wiki kadhaa Umoja wa Mataifa umepata taarifa za kuaminika za usambazaji wa silaha na sare za kijeshi kwa vijana wa chama tawala Imbonerakure, shutuma ambazo zimetupiliwa mbali na serikali ya Burundi.

Wakaazi wa mji wa Bujumbura wakitiwa hofu na hali inayojiri kufuatia onyo la UN dhidi ya serikali ya Burundi.
AFP
Burundi inapitia wakati huu mgogoro mkubwa wa kisiasa kutokana na mgawanyiko kati ya chama cha rais Pirrea Nkurunzia, chenye wahutu wengi na chama cha UPRONA, chenye watutsi wengi.
Bunge la Burundi lilikataa katikati ya mwezi wa machi kuidhinisha mswada wa sheria ya kufanya marekebiho ya katiba, ambayo kwa mujibu wa upinzani ingelisababisha taifa hilo kuingia katika dimbwi la machafuko ya kikabila kama yale yaliyoshuhudiwa katika miaka ya 1993-2006.
Vyombo vya sheria vya Burundi viliwahukumu hivi karibuni kifungo cha maisha jela wafuasi 21 wa chama cha upinzani cha MSD kwa kuwatuhumu kwamba “walianzisha vurugu wakitumia silaha”, baada ya makabiliano na polisi ambayo iliwakatila wasifanye mazowezi ya kukimbia, wakati vijana wa chama tawala wamekua wakifanya mazoezi hayo kila jumamosi.

No comments: