Tuesday 1 April 2014

Uongo Mtupu simba hatuja hongwa ilitufungwe na Azam

KOCHA wa Simba Zdravko Logarusic, ameshangazwa na taarifa kwamba kikosi chake kilipanga matokeo dhidi ya Azam FC kwa kusema hilo haliwezi kufanyika chini ya utawala wake.

Akizungumza na Mwanaspoti Logarusic, alisema ameshangazwa na taarifa kwamba kikosi chake kilikuwa na lengo la kujirahisisha kufungwa katika mchezo huo wa juzi, lakini hilo haliwezi kufanyika chini ya utawala wake na kila mtu aliona jinsi vijana wake walivyopambana.

“Kulikuwa na kelele nyingi kwamba tuliingia uwanjani na akili ya kwamba tuwape ushindi kirahisi Azam, mimi ni kocha siwezi kuruhusu kitu cha namna hiyo kufanyika katika timu yangu, tulitawala mchezo kwa asilimia 60,tulikuwa vizuri kuliko wao, tuliwazidi kimbinu mwisho wakatumia makosa yetu kushinda,” alisema Logarusic

“Watu wanaweza kuzungumza chochote wanachoweza kusema lakini katika mazingira rahisi ni vigumu kukubali maneno hayo ukilinganisha na jinsi wachezaji wangu walivyocheza.”

Katika hatua nyingine, Logarusic alisema anashindwa kushiriki kwa nguvu zote katika kusaidia majukumu ya kusaka nyota wapya wa msimu ujao kutokana na kutojua hatima yake katika klabu hiyo ingawa alikiri kuanza mazungumzo na uongozi.

“Kwa sasa kuna wachezaji ambao tumewapata natakiwa kuwafuata huko waliko kujiridhisha juu ya viwango vyao, yapo mengi ambayo natakiwa kuyafanya lakini kikwazo ni kutojua hatma yangu hapa Simba,” alisema Loga.

“Najua kuwa Ghana kuna wachezaji wawili watatu naweza kwenda kuwaangalia kwa sasa akiwemo mshambuliaji nashindwa kuanza mchakato huo kutokana na hili la mkataba, nikijua kama nitakuwa hapa naweza kwenda nma kuweka wazi taarifa zake,”alisisitiza

No comments: