Wednesday 16 April 2014

Walionadilisha jinsia India kutambuliwa Kisheria sasa

Watu wa jinsia ya tatu India.

Watu wa jinsia ya tatu India. Mahakama kuu ya India imeamua kuwatambua rasmi kisheria watu waliobadili  jinsia zao na kuwapa haki sawa na kuwatambua kama jinsia ya tatu Maamuzi hayo ya kihistoria  yanaelekeza serikali kuu na za majimbo kuwajumuisha watu waliobadili jinsia zao katika mipango ya misaada ya serikali  kwa watu masikini.

Nyaraka zote rasmi za kikazi zinatakiwa kuwa na kipengele cha watu waliobadili jinsia pamoja na kuwa na mwanamke na mwanaume.

Wanaharakati walisifia maamuzi hayo  wakisema yatasaidia kutoa haki sawa kwa kundi ambalo limenyimwa haki katika nchi hiyo.

No comments: