Monday 21 April 2014

Wanajeshi 11 wa Algeria wauawa katika shambulio la kuvizia

Milima ya Ouacifs, nchini Algéria, ambako waliuawa wanajeshi wa Algeria juzi jumamosi, aprili 19.
Milima ya Ouacifs, nchini Algéria, ambako waliuawa wanajeshi wa Algeria juzi jumamosi, aprili 19.

Wanajeshi 11 wameuawa, baada ya msafara wa magari ya kijeshi kushambuliwa katika eneo la Kabylie kwenye milima ya Ouacifs katika wilaya ya Tizi Ouzou nchini Algeria siku tatu tu baada ya uchaguzi wa urais kufanyika nchini humo.

Wizara ya ulinzi imethibitisha kwamba wanajeshi 11 wameuawa katika shambulio hilo.
Lakini vyombo vya habari vimeeleza kwamba wanajeshi 16 ndio wameuawa. Miaka mitatu iliyopita wanajeshi 14 waliuawa katika eneo la Kabylie katika shambulio la kuvizia
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi, shambulio la jumamosi lilitokea saa 3 na dakika 15 usiku saa za Algeria (sawa na saa 2 na dakika 15 za kimataifa).
Shambulio hilo lilikua limelenga kikosi cha wanajeshi wa eneo la Tizi Ouzou ambao “walikua wakifanya ulinzi wa uchaguzi wa urais”.
Wizara ya ulinzi imewachukulia watu waliendesha shambulio hilo kama magaidi, huku ikibaini kwamba shambulio hilo linaonyesha uwajibikaji wa jeshi la Algeria kwa kutokomeza makundi ya kigaidi.
Wizara ya ulinzi imeendelea kusema kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka 2014, wanamgambo 21 wa kislamu waliuawa katika eneo hilo, ambalo lilikua hatari miaka mitatu iliyopita, kwa vitendo vya ugaidi.
Shambulio hili linaelezwa kuwa baya miongoni mwa mashambulizi yaliyowahi kutokea katika eneo la kabylie, miaka mitatu iliyopita, ambapo wanajeshi 14 waliuawa katika shambulio dhidi ya kambi ya jeshi.
Wakati huohuo, duru za usalama ziliyotajwa na kituo cha habari cha Algeria APS zimefahamisha kwamba wanamgambo wawili waliuawa jana jioni katika mkoa wa Abdelmadjid karibu kilomita 300 na mji wa Algiers.

Abdelaziz Bouteflika , akiwa kwenye kiti cha magurudumu, karibu yake kushoto ndugu yake akiwa pia mshauri wake, Saïd, wakati wa uchaguzi wa aprili 17.
AFP PHOTO / FAROUK BATICHE
Hayo ya kijiri, rais Abdelaziz Bouteflika ambaye anaonekana kuwa muasisi wa maridhiano ya kitaifa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya tisini, ndiye aliyechaguliwa tena kuwa rais kwa awamu ya nne mfululizo, akishinda kwa asilimia 81 ya kura.
Umoja wa Afrika ambao umepeleka waangalizi wapatao 200 nchini kote unazungumzia uchaguzi huo kuwa wa haki licha ya madai ya wagombea wengine ambao wanatofautiana na matokeo hayo, akiwemo Ali Benfils, ambae alitangaza kwamba hatakubaliana na matokeo ya uchaguzi.

Ali Benflis, ambae aligombea uchaguzi wa urais nchini Algeria aprili 17 mwaka 2014.
REUTERS/Louafi Larbi
Awali Benfils alifahamisha kwamba uchaguzi huo wa urais nchini Algeria uligubikwa na wizi wa kura.

No comments: