Tuesday 13 May 2014

17 wafa katika shambulio la bomu Somalia

Shambulizi la kujitoa mhanga katika mji wa Baidoa limewauwa watu 17 huku wengine 20 wakijeruhiwa.
watu-17-wafariki-katika-shambulizi-la-bomu-so
Kulingana na habari iliyotolewa na walioshuhudia shambulizi hilo, watu wawili walitekeleza shambulizi la kujitoa mhanga kwa kulipua gari lililokuwa limebeba mabomu. Watu hao wawili walifariki pamoja na wengine 15 huku wengine 20 wakijeruhiwa vibaya.
Ripoti ilisema kuwa huenda idadi ya waliofariki kutokana na shambulizi hilo ikaongezeka kwa kuwa eneo lililolipuliwa lilikuwa na watu wengi.
Serikali ya Somalia bado haijatoa ripoti rasmi kuhusiana na shambulizi hilo ingawa hakuna pande iliyodai kuhusika na shambulizi hilo.

No comments: