Sunday 18 May 2014

Arsenal yachukua Kombe la FA

Arsenal yaicharaza Hull City katika mechi ya fainali ya FA Cup.
arsenal-yachukuwa-kombe-la-fa-cup
Timu ya Arsenal na Hull City zilichuana katika kinyang’anyiro cha kuwania kombe la FA Cup Uingereza.
Timu ya Arsenal iliyopania kumaliza ukame wa kutochukuwa kombe kwa miaka 9, walianza mechi vibaya baada ya kufungwa na Hull City katika dakika 3 kupitia mchezaji James Chester na Curtis Davies katika dakika ya 9.
Arsenal ilifanikiwa kufufua matumaini yake baada ya mchezaji Santi Carzola kufunga katika dakika ya 17 na kuwawezesha Hull City kukamilisha kipindi cha kwanza wakiongoza 2 – 1.
Katika kipindi cha pili Arsenal walicheza kwa mashambulizi zaidi hadi kuweza kupata bao la pili kupitia Laurent Koscielny  katika dakika ya 71.
Mechi ilikamilika  2 – 2 katika muda wa kawaida. Kwenye muda wa ziada, Arsenal ilzidisha mashambulizi na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia Aaron Ramsey na kukamilisha mechi 3 – 2.

No comments: