Sunday 18 May 2014

Athletico De Madrid mabingwa wa La Liga 2013/2014

Athletico Madrid wanyakuwa ubingwa wa ligi kuu ya Uhispania ya La Liga baada ya kutoa sare katika mechi dhidi ya Bracelona.
athletico-madrid-ndio-mabingwa-wa-la-liga
Timu hiyo ya Athletico Madrid , imenyakuwa ubingwa huo baada ya miaka 18.
Timu ya Athletico Madrid imekamilisha msimu wa 2013 – 2014 kwa alama 91baada ya kutoka sare ya 1 – 1  na Barcelona katika mechi ya mwisho ya La Liga.
Athletico Madrid walianza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya wachezaji wao Diego Costa na Arda Turan kupata majeraha katika dakika ya 13 na 20 na kuwalazimu kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili.
Barcelona iliweza kukamilisha kipindi cha kwanza kwa uongozi wa bao 1 – 0 baada ya mshambuliaji Alexis Sanchez kutia kimyani bao la kipekee katika dakika ya 33. Kipindi cha pili katika dakika ya 49, Diego Godin alifanikiwa kufunga bao lilioweza kuwaletea Athletico Madrid ubingwa wa La Liga.
Kwa dakika zilizosalia, mchuano ulizidi kupamba moto na timu zote mbili ziliweza kupata nafasi za wazi bila ya mafanikio. Mechi iliisha 1 – 1. Baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho, wachezaji pamoja na mashabiki wa Athletico Madrid walianza kusherehekea ubingwa wao huku wakipewa pongezi na mashabiki wapatao elfu 100 waliohudhuria katika mechi hiyo Nou Camp

No comments: