Friday 30 May 2014

Boko haramu wateka viongozi wawili

Watu  wenye  silaha wanaoshukiwa  kuwa  ni  kutoka  kundi la  Kiislamu  la  Boko  Haram wamewateka  nyara  viongozi wawili wa   kikabila  wa  Kiislamu  kaskazini  mashariki  ya Nigeria  leo.  Watu  hao  wenye  silaha  wamewateka mtawala  wa  eneo  la  Gwoza, Alhaj Idriss Timta , na mtawala  wa  Uba, Alhaj Ismaila Mamza, waliokuwa  katika magari  yao  katika  mji  wa  Zhur, eneo  la  ndani  katika eneo  la  kusini  mwa  jimbo  la  Borno. Duru  za  kiusalama na  afisa  wa  jimbo  la  Borno  ameliambia  shirika  la habari  la  Reuters  kuwa  watu  hao  walikuwa  wakielekea katika  mazishi.  Duru moja  ilisema  kuwa  jeshi  limewekwa katika  eneo  hilo  kuwatafuta  mateka , licha  ya  kuwa ujumbe  kama  huo  kila  mara  huambatana  na  hatari kubwa.

No comments: