Saturday 17 May 2014

China yaitaka Vietnam ilinde usalama wa kampuni na watu wa China nchini Vietnam

Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi jana usiku alizungumza na naibu waziri mkuu wa Vietnam ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje ya nchi hiyo Bw. Pham Binh minh kwa njia ya simu, ambapo aliilaani vikali Vietnam kutokana na vitendo vya kushambulia kampuni za China vinavyotokea nchini Vietnam. Hivi karibuni mashambulizi dhidi ya wawekezaji kutoka nje yalitokea nchini Vietnam, baadhi ya kampuni za China, Singapore na Korea Kusini zilishambuliwa, na kusababisha kifo cha raia mmoja wa China, wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, na hasara kubwa ya mali.

Bw. Wang Yi amesema Vietnam inapaswa kuwajibika na mashambulizi dhidi ya kampuni na watu wa China, na China inaitaka Vietnam ichukue hatua zenye ufanisi, kuzuia vitendo vya kimabavu, kulinda usalama wa kampuni na watu wote wa China, kuwatibu majeruhi, kuanza uchunguzi kuhusu mashambulizi hayo, kuwaadhibu wahalifu wote, na kutoa fidia kwa kampuni na watu walioathiriwa.
Naye Bw. Pham Binh Minh amesema, Vietnam imewakamata watuhumiwa zaidi ya 1000, na itachukua hatua zote kulinda usalama wa kampuni na watu wa China nchini humo.

No comments: