Saturday 17 May 2014

Hadi sasa imefikia idadi yaWatu 10 waliokufa kutokana na mlipuko Nairobi


Mlipuko wa bomu ndani ya soko la Gikomba Nairobi May 16 2014
Mlipuko wa bomu ndani ya soko la Gikomba Nairobi May 16 2014

Habari za awali kutoka Nairobi zinaeleza kwamba karibu watu 10 wameuliwa na wengine wengi kujeruhiwa wakati milipuko miwili ya bomu ilitokea katika mtaa wa soko la Gikomba.

Polisi wasamema bomu la kwanza ililipuka ndani ya gari la abiria la "matatu", na bomu la pili lilitokea  ndani ya soko la Gikomba. Idadi halisi ya majeruhi haijulikani bado wakati watumishi wa afya wakiwapeleka baadhi hospitali za karibu.

Rais Uhuru Kenyatta aliyekua anahutubia taifa wakati bomu lilipotokea ametoa rambi rambi zake kwa walouwawa na kuahidi kwamba watafanya kila wawezalo kun'gowa ugaidi nchini Kenya.

Rais Kenyatta alitoa wito kwa washirika wa nchi yake kufanya kazi pamoja kusaidia kupambana na magaidi wanaojaribu kuleta hasara katika nchi yake.

Mapema wiki hii katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya kenya alizilaumu baadhi ya nchi za magharibi zilizotoa onyo kwa raia wake kujitahadhari akisema hatua hiyo inaharibu sifa ya nchi yake.

Inavyoonekana Marekani, Uingereza, Australi na Japan huwenda zilikuwa na habari hizo za kuaminika za kutokea shambulio la kigaidi, ndio maana zilitoa onyo hilo mapema wiki hii.

Mwandishi ukomboz mjini Nairobi anaripoti kwamba ndege mbili maalum ziliwasili Nairobi leo na kuwasafirisha watali walokuwa hawajamaliza ziara yao.

No comments: