Tuesday 13 May 2014

Jeshi la Israel lakiri kuwa haliko tayari kuingia vitani

Jeshi la Israel lakiri kuwa haliko tayari kuingia vitaniMaafisa zaidi ya 20 wa ngazi za juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuandikia barua Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu na kumueleza kwamba jeshi la nchi hiyo haliko tayari kupigana kwenye vita vyovyote vile. Gazeti la Yediot Aharonot la utawala wa Israel limefichua habari hizo na kuandika kwamba, maafisa hao wa ngazi za juu jeshini wamemueleza Waziri Mkuu , Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Uchumi kwamba jeshi hilo haliko tayari kuingia kwenye vita na nchi yoyote ile. Taarifa iliyotolewa na maafisa hao imeeleza kwamba, licha ya kupita miaka mitatu na nusu ya mazoezi  kamambe ya kijeshi lakini jeshi hilo bado halijawa tayari kuingia vitani. Maafisa hao wamesisitiza kuwa, kujitosa kwenye vita bila ya kuwa na maandalizi ya kutosha ni sawa na kujitangazia kifo. Maafisa hao wameeleza kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaamua kuingia kwenye vita na nchi za Kiarabu, utakabiliwa tena na fedheha iliyoukumba mwaka 1973. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Waziri Mkuu wa Israel mara kadhaa amenukuliwa akitoa vitisho vya kutaka kuishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Viongozi wa Iran wamesisitiza kuwa, iwapo utawala huo utajaribu kuleta chokochoko na kuishambulia kijeshi Iran utakiona cha mtema kuni.

No comments: