Wednesday 14 May 2014

Kiongozi wa Boko Haram kauwawa

Msemaji wa huduma ya siri ya polisi wa Nigeria, Marilyn Ogar alitoa taarifa inayohakikisha kuuawa kwa kiongozi wa Boko Haram, Abu bakr Sekai.
madai-ya-kuuawa-kwa-kiongozi-wa-boko-haramu
Ogar alisema katika mkutano wa waandishi wa habari ya kuwa kundi la Boko Haram limekuwa jina la bidhaa, wanaweza kujitokeza wakati wowote wakitumia jina lolote. Alihakikisha kwamba kiongozi wao, Abu Bakr Sekai alikuwa ameuawa.
Marilyn Ogar alisisitiza pia ya kwamba hakuna haja ya kushuku taarifa iliyotolewa na vikosi vya usalama.
Jana katika video iliyotiwa mkononi na gazeti la Daily Trust, alionekana wazi mtu anayedaiwa kuwa Sekai akidai kuachiliwa kwa wanachama wa Boko Haramu walioko jela iwapo wataachiliwa huru wasichana waliotekwa nyara.
Sekai, anaezungumza Kiarabu, Kiingereza na lugha za asilia za Hausa pamoja na Kanuri alisemekana kuwataka baadhi ya wasichana kuikubali dini ya Kiislamu

No comments: