Thursday 22 May 2014

Kura ya kuipeleka kesi ya Syria kwa ICC yapingwa na Urusi

Baraza la Usalama
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeshindwa kupitisha azimio la kuipeleka kesi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita nchini Syria kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.
Nchi kumi na tatu wanachama wa Baraza hilo zimeunga mkono mswada wa azimio hilo, lakini kwa sababu ulipingwa na Urusi, mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama, huku Uchina ikionyesha kutoegemea upande wowote, mswada huo haukupitishwa.
Mapema kabla ya kura hiyo, ujumbe wa Katibu Mkuu kwa Baraza la Usalama ulisisitiza kuwa uwajibikaji kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaweza kuzuia ukatili zaidi nchini Syria. Ujumbe wa Bwana Ban umesomwa na Naibu wake Jan Eliasson kwa Baraza la Usalama la Umoja

No comments: