Monday 26 May 2014

Mbeya city waanza vyema Michuano ya CECAFA wachapa 3 2 Academie Tchite

IMG_7961 WAGONGA Nyundo wa jijini Mbeya, Mbeya City fc jana walitoka  kushinda mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi katika mchezo wa kundi B wa michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea mjini Khartoum nchini Sudan.

Mbeya City fc waliofika Khartoum siku moja kabla ya mechi walianza kufungwa bao katika dakika ya 10 baada ya Rashid kumtungua kipa wao, lakini walirudi mchezoni baada ya Paul Nonga kusawazisha bao hilo dakika 5 baadaye. 


Dakika ya 27, nahodha wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya kama ilivyo kawaida yake alifunga bao la pili kwa njia ya kichwa. Them Felix `Mnyama` alihitimisha karamu ya mabao dakika ya 37 baada ya kufunga bao safi na kuwapeleka Mbeya City mapumziko wakiwa na furaha.

Kipindi cha pili, Waburundi walikuja na Presha kubwa na katika dakika ya 68  Manirakiza alifunga bao la pili.

IMG_8009

Kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi aliwapongeza vijana wake kwa ushindi na kuahidi kufanya vizuri mchezo unafuata.

“Vijana walipunguza kasi kipindi cha pili, lakini nawasifu kwa kuvuna pointi tatu muhimu”. Alisema Mwambusi.

Mpinzani wake,  Ndayizeye Jimmy aliwapongeza  Mbeya City kwa soka safi.

Wafungaji wa mabao: Academie Tchite: (Rashid Patient-10’, Manirakiza 68’).

Mbeya City: (Nonga paul-15’, Mwagane Yeya 27’ and Themy Felix 37’).

Mchezo mwingine ulipigwa kuanzia majira ya saa 2:00 usiku na kushuhudia AFC Leopard ya Kenya ikiibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Etincelles.

No comments: