Sunday 25 May 2014

Real Madrid Bingwa UEFA

Timu ya Real Madrid yaicharaza Athletico Madrid katika mechi ya fainali ya kuwania kombe la UEFA.
real-madrid-ndio-mabingwa-wa-ulaya
Real Madrid ilinyakuwa ushindi wa ligi kuu ya mabingwa wa Ulaya baada ya kuishinda Athletico Madrid kwa mabao 4 – 1 katika mechi iliyoendelea hadi muda wa ziada..
Mechi hiyo ya kihistoria iliyoleta pamoja timu mbili zinazotoka mji mmoja kwa mara ya kwanza katika miaka 59 ya fainali za makombe ya Ulaya, ilikuwa ya kusisimua ilipofikia dakika ya 90 + 3.
Hadi kufikia dakika hiyo, matumaini ya timu ya Athletico Madrid iliyokuwa ikiongoza kwa bao 1 – 0 na kujiandaa kupokea ubingwa wa Ligi Kuu ya Ulaya, yalivunjwa baada ya mchezaji machachari wa Real Madrid Sergio Ramos kukomboa bao kwa kichwa.
Bao hilo lilisababisha mechi hiyo kumalizika sare katika muda wa kawaida na kulazimika kuongezwa muda wa ziada uliowezesha Real Madrid kunyakuwa kombe hilo kwa mara ya 10 baada ya kushinda 4 -1.
Bao la Athletico Madrid lilfungwa na Diego Godin katika dakika ya 35 ilhali mabao ya Real Madrid yalifungwa na Sergio Ramos dakika ya 90+3, Gareth Bale dakika ya 110, Marcelo dakika ya 118 na Cristiano Ronaldo dakika ya 120 kupitia mkwaju wa penalti.
Silverware: Captain Iker Casillas lifts the Champions League trophy for Real MadridNahodha Iker Casillas akinyanyua kombe
Uplifting: Ronaldo gets his hands on the trophy in Lisbon after Real's extra time victory Ronaldo akinyanyua kombe mjini  Lisbon baada ya  Real kushinda dakika za nyongeza
Ronaldo na Bale  wakifurahia ushindi wa Real Madrid
Wachezaji wa  Real Madrid wakishangilia ubingwa wao wa 10
HATIMAYE Gareth Bale ameisaidia Real Madrid kutumiza ndoto za `La Decima` baada ya kutwaa ndoo ya 10 ya UEFA kufuatia ushindi wa dakika za nyongeza katika mchezo wa fainali dhidi ya majirani zao Atletico Madrid.
Alizaliwa Wales, alikulia Southampton na kung`ara Tottenham, nyota huyo mwenye miaka 24 ameendelea kuonesha kuwa Real Madrid hawakukosea kumsajili kwa rekodi ya dunia baada ya kufunga bao ambalo limeandikwa katika historia ya klabu. Bale alionekana kutokuwa makini kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi za kufunga, lakini aliendeleza rekodi nzuri ya msimu wake wa  kwanza Real Madrid baada ya kuifungia bao la pili katika dakika za nyongeza, kabla ya vijana hao wa Carlo Ancelotti kushinda kwa mabao 4-1. Kikosi cha Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao (Marcelo 59), Modric, Khedira (Isco 59), Di Maria, Bale, Benzema (Morata 79), Ronaldo.
Wachezaji wa akiba: Diego Lopez, Pepe, Arbeloa, Illarramendi.
Waliopata kadi za njano: Ramos, Khedira, Marcelo, Ronaldo, Varane.
Waliofunga magoli. Ramos 90, Bale 110, Marcelo 118, Ronaldo 120. Kikosi cha Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis (Alderweireld 83), Raul Garcia (Sosa 66), Gabi, Tiago, Koke, Villa, Diego Costa (Adrian 9).
Wachezaji wa akiba: Aranzubia, Mario Suarez, Rodriguez, Diego.
Mfungaji wa Goli: Godin 36.
Walioneshwa kadi nyekundu: Garcia, Miranda, Villa, Juanfran, Gabi, Koke, Godin.
Mwamuzi: Bjorn Kuipers (Holland)

No comments: