Tuesday 27 May 2014

walipo fichwa wasichana waliotekwa NIgeria yajulikana

sehemu-walipofichwa-wasichana-waliotekwa-nyarMkuu wa wafanyakazi nchini Nigeria, Alex Badeh alitoa taarifa

Mkuu wa wafanyakazi nchini Nigeria, Alex Badeh amesema kulingana na wanamgambo wa Boko Haram wameonyesha sehemu walipowaficha wasichana.
Katika taarifa aliyoitoa kwa waandamanaji waliojikusanya mjini Abuja, Badeh "tunajua walipo mabinti zenu ila hatutowaambia nyinyi. Hatuwezi kuwapatia siri za kijeshi. Tunafanya kazi, na tutawapatia mabinti wenu." Alisema. Ili kuweka maisha yao katika usalama, jeshi linapanga operesheni kabambe na ya ustadi ya uokoaji, alibainisha Badeh. "Hatutakiwi kumuambia mtu yeyote kwamba jeshi litafanya nini", alisema.
Kwa upande mwingine, Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, limeeleza kuwa serikali ya Nigeria imefikia mazungumzo baina yake na Boko Haram. Kwa mujibu wa BBC, katika mazungumzo, ili kuwaacha wasichana huru, wametaka wanachama 100 wa Boko Haram waachiwe huru kutoka gerezani. Hata hivyo serikali ya Nigeria ilikataa mpango huo.

No comments: