Saturday 7 June 2014

Bonanza la kuapisha mwawaziri TICD-Tengeru lafanyika leo



Bonanza la kuapishwa kwa Mawaziri wa chuo kikuu cha maendeleo ya jamii Tengeru  limefanyika leo hukulililokuwa limegubikwa na michezo ya aina mbali mbali kama vile ukimbizaji wa kuku,Volleyball(mpira wa wavu) na Mpira wa miguu .Katika Bonanza hilo mawaziri walio apishwa ni pamoja na waziri wa Elimu (Erick Eponda) Afya na Mazingira (BeatriceKaranja ) Michezo na utamaduni (Emmanuel na naibu wake Goodbless Lema naLoserian Moleli, Sheria na Katiba (Lule )  waziri wa Mikopo Makali Lyaki na naibu wake ni Loserian Molel.

 Katika uapishwaji huo mchezo ulio wavutia wengi ni mpira wa miguu ambao ulishindanisha Timu toka chuo hapa Chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru (TICD) na timu alikwa toka chuo cha Kilimo Tengeru (LITA)
Katika Mchezo huo ulio pigwa katika kiwanja cha Chuo cha LITA ulikuwa ni wakusisimua na wenye mvuto ambapo kila timu iliingia uwanjani zikiwa zimekamiana na kila timu ikihitaji ushindi
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi huku timu zote mbili zikiwa zinalisakama lango la mwenzie mnamo dakika ya 40 ya mchezo nusura LITA wajipatie bao la kuongoza baada ya kiungo mkabaji wao kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa TICD na kugonga mwamba hadi mapumziko TICD 0 0 LITA
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Timu ta TICD ikianza kwa kasi na kwakushambulia lango la LITA huku mshambuliaji wa TICD Goobless Lema akionekana Mwiba kwa mabeki wa Lita , Mnamo Dakika ya 68 Mshamuliaji hatari Goodbles Lema alitoa pasi ya mwisho kwa Herndricos  Twinzi  alimaarufu kwa jina la Chicharito na kutumbukiza mpira nyavuni na kufanya TICD kiongoza kwa bao 1
Hata hivyo LITA haikukata tama ilijikakamua na kulishambulia lango la TICD mara kwa mara bila Mafanikio ,, Mnamo dakika ya 72 ya mchezo TICD walifanya mabadiliko kwa kumtoa Sixbert jezi namba 9 na kumwingiza Deogratius jezi namba 14 . Mabadiliko haya yaliongeza ladha ya mpira na kufanya mpira uwe wa kazi na wakushambuliana kwa zamu
Mnamo dakika ya 85 LITA walielekeza mashambulizi makali kwenye lango la TICD mshambuliaji Elia wa LITA alitoa pasi kwa mshambuliaji hatari wa LITA aliyekuwa akiisumbua ngome ya TICD kwajina alifahamika kama Kabamba aliyepiga shuti na kupaa sentimita chache juu ya lango la TICD ambapo mwamuzi wa mchezi huo alishindwa kuona vyema na kuamuru kuwa ni goli , Hata hivyo washika vibendera walipingana na mwamuzi  wa kati na kupelekea mwamuzi huyo kubadili mawazo yake na kusema mpira upigwe kama kona ambapo wachezaji wa LITA walipingana na mawazo ya mwamuzi huyo na kuleta vurugu ambapo ulipelekea mchezo kuvunyika mnamo dakika ya 87 , Hadi kuvunjika kwa mchezo TICD 1 0 LITA


No comments: