Friday 13 June 2014

Brazil waanza Michuano ya kombe la dunia vyema wailaza Croatia 3-1

Neymar alifunga mabao mawili Brazil iipoilaza Croatia 3-1

Wenyeji wa kombe la dunia Brazil walitoka nyuma na kuilaza Croatia mabao 3-1 katika mechi ya kufungua fainali ya dimba la mwaka huu iliyochezwa katika uwanja wa Sao Paolo (Arena de Sao Paulo).
Mechi hiyo ilikuwa ikitizamwa na mashabiki 65,000 uwanjani humo baada ya kushuhudia tafrija ya ufunguzi iliyotizamwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja kupitia kwa runinga
Wenyeji Brazil walitazamiwa kufunga bao la kwanza mapema katika mechi hiyo lakini uwanjani mambo yalikuwa tofauti ,Marcelo alijifunga mwenyewe na kuiweka Croatia mbele baada ya dakika 11 pekee ya kipindi cha kwanza .
Wenyeji waliotamaushwa na bao hilo walikuwa na matumaini kuwa kiungo machachari anayechezea Barcelona ya Uhispania Neymar atawaongoza ''the samba boys'' kutwaa taji lao la sita la dunia nyumbani.
Na nyota huyo hakuboronga alitumia kila mbinu ikiwemo kumbo iliyompelekea kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano na refarii kutoka Japan Yuichi Nishimura.
Hata hivyo dakika chache tu baada ya kuonyeshwa kadi hiyo ya njano Neyma alijifurukuta na kuisawazishia Brazil katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 22 aliiweka Brazil Mbele zikiwa zimesalia dakika 19 mechi hiyo kukamilika baada ya refarii kutoka Japan
Nishimura kupiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango.
hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred.
Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi mjapan huyo kuwa haikuwa kweli fred alikuwa amejiangusha lakini maoni yao hayakusikika.
Cameroon kukabiliana na Mexico hapo kesho

Neymar kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo aliiweka Brazil mbele kufuatia mkwaju huo wa penalti.
Vijana wa Luiz Scolari hawakuwachia hapo waliendelea kushambulia lango la Croatia na juhudi zao zilizaa matunda katika kipindi cha ziada Oscar alipompata kipa wa croatia ameduwaa na kufutamatisha kichapo hicho kunako dakika ya 91 .
Kufuatia ushindi huo wenyeji hao sasa wamejikita katika nafasi ya kwanza katika kundi A wakiwa na alama tatu.
Cameroon na Mexico zinashikilia nafasi ya pili na tatu katika kundi hilo .
Timu hizo zitakabiliana hapo Kesho.

No comments: