Wednesday 11 June 2014

Israel wapata rais mpya

Reuven Rivlin ndiye Rais mpya wa Israel
Aliyekuwa spika wa Bunge la Israel Reuven Rivlin amechaguliwa kuwa rais wa 10 wa Israel.
Reuvin alipata kura 43 katika awamu ya kwanza na 63 katika awamu ya pili huku mpinzani wake Meir Sheetrit akipata kura 53 katika uchaguzi uliofanywa katika Bunge la Israel.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Spika wa bunge, Yuli Edelshtein alisema, " Rivlin amechguliwa kuwa rais."
Miaka 7 iliyopita Rivlin aliwahi kugombania kiti cha urais nakuibuka wapili nyuma ya rais anayeondoka Shimon Peres. Rivlin aliyepigiwa upato wa kushinda uchaguzi huu na vyombo vya habari alihudumu kama Spika wa bunge ya Israel kwa mihula miwili.

No comments: