Friday 27 June 2014

Jasmin Sudi awaomba wanachama wa Simba wamchague

Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Jasmin Sudi amewaomba wanachama wamchague ili aendeleze soka na kurudisha heshima ya mwanamke iliyopotea katika klabu hiyo.
Akizungumza na mwandishi wetu hili Dar es Salaam jana, Jasmin alisema jambo la kwanza atakalofanya ni kurudisha nguvu ya umoja wa wanawake wa Simba kwa kufanya nao kazi kwa karibu.
“Umoja wa wanawake ni muhimu katika klabu yetu kwani ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Simba, lakini kwa siku za karibuni kundi hili limekuwa nyuma,” alisema.
Mgombe huyo alijinadi kuwa atalinda katiba ya Simba na kudumisha uhusiano mzuri baina ya matawi na wanachama wote wa klabuni hapo.
Alisema kwa kipindi cha miaka saba aliyofanya kazi kama katibu muhtasi wa klabu hiyo, amejifunza mengi na atakuwa mshauri mzuri kwa rais ajaye iwapo atachaguliwa kuwa mjumbe katika Kamati ya Utendaji, huku mkazo wake ukiwa katika soka.
Jasmin, ambaye ni mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa alibainisha kuwa maneno bila vitendo katika klabu yoyote ya soka, ni kujidanganya kwani mwisho wa siku soka linatakiwa lionekane.
“Simba kama klabu haiwezi kuwa imara bila kuhakikisha mpira unachezwa kwa kiwango cha juu uwanjani, hivyo ili kuhakikisha hilo linatimia ni vema kuchagua viongozi wa mpira na si wa maneno.
“Chagueni viongozi wapenda mpira, msichague wapenda ofisi na majigambo. Wapenzi na wadau wa soka hawataki maneno wanataka mpira siyo tu kuwapo bali kuonekana unachezwa kwa kiwango na hadhi ya timu yenye miaka mingi kama Simba,” alisema.
Jasmin aliongeza kuwa wakati wa kucheza soka la kelele na fitina umekwisha kutokana na kuwapo kwa upinzani wa kweli kwenye soka, hivyo wanachama wanapofanya uchaguzi walitilie maanani suala hil

No comments: