Wednesday 4 June 2014

Jenerali anusurika katika mlipuko


Jenerali muasi anusurika shambulizi la Bomu

Mlipuaji wa kujitioa mhanga ameshambulia nyumba ya jenerali muasi ambaye amekuwa akiongoza kampeni za kijeshi dhidi kundi la wapiganaji wa kislamu wanaoungwa mkono na serikali nchini Libya ambao watu wanne waliuawa.
Jenerali Khalifa Haftar alinusurika shambulio hilo lililotekelezwa kwenye jengo moja la shambani kwenye mji wa Abyar karibu kilomita sitini mashariki mwa Benghazi.
Watu kadha walijeruhiwa.
Vikosi vya Jenerali Haftar vimekuwa vikiendesha kampeni dhidi ya wapiganaji wa kiislamu mjini Benghazi kwa kipindi cha majuma matatu sasa.
Haftar ambaye alikuwa mkuu wa majeshi wakati wa utawala wa rais wa zamani Muammar Gaddafi anaishutumu serikali kwa kuunga mkono ugaidi madai yanayokanushwa na serikali.
Mlipuaji wa kujitolea mhanga amlenga Jenerali muasi
Mshambuliji wa kujitoa mhanga aliendesha gari lililokuwa limejazwa milipuko kwenda kwa nyumba ya Jenerali huyo Jumatano.
Jenerali Sager AL-Jarushi ambaye ni kamanda wa ngazi za juu na mshirika wa karibu wa Jenerali Haftar aliwambia waandishi wa habari kuwa wanne kati ya walinzi wake waliuawa kwenye shambulizi hilo.
Watu wengine 20 wanaripotiwa kuuawa kwenye mapigano makali kati ya vikosi vya Jenerali Haftar na wapiganaji wa kislamu mjini Benghazi .

No comments: