Saturday 7 June 2014

Kiongozi wa kiidini Nigeria aaga dunia


Amiri wa jimbo la Kano Ado Abdullah Bayero ameaga dunia  akiwa na umri wa miaka 83

Amiri huyo aliyeongoza jimbo la Kano kwa kipindi cha nusu karne alikuwa maaarufu na mwenye kuheshimika kama kiongozi wa jamii ya waislamu. Amiri Bayero alijulikana pia kwa upinzani wake dhidi ya waasi wa Boko Haram ambao wanaendelea kumwaga damu nchini Nigeria.Mwaka jana Amiri Bayero alinusurika shambulizi la wanamgambo wa Boko Haram lililowauwa walinzi 4 waliokuwa katika msafara wake. Safari yake ya Uingereza kwa ajili ya matibabu muda mfupi baada ya shambulizi hilo liliwatia wengi shaka.
Cheo cha Amiri wa Kano kilikuwa maarufu sana katika eneo hilo kama mamlaka ya kiislamu

No comments: