Sunday 1 June 2014

Mwanafunzi UDSM afia hostel

Sekabenga MwakimenyaWATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti jijini Dares Salaam akiwemo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Sekabenga Mwakimenya (22) kukutwa amekufa chumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni (RPC), Camillus Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba mchana katika chumba namba 110 alichokuwa akiishi katika kampasi ya Nyerere, mwili ukiwa hauna jeraha lolote.
Wambura alisema mwanafunzi huyo  alikuwa akisoma kozi ya uhasibu na biashara chuoni hapo na kwamba sababu za kifo chake hazijafahamika.
Katika tukio jingine, Wambura alisema mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Jabir Joseph,  anayekadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 30, alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake.
Alisema Jabir, ambaye ni mkazi wa Mabibo Makutano, alijinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali ambayo aliifunga kwenye nondo ya dirisha la chumba hicho.
Wambura alisema mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa unaning’inia kitandani na polisi haimshikilii mtu yeyote kuhusiana na matukio yote mawili huku maiti zote zimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

No comments: