Wednesday 11 June 2014

Ugojwa wa ajabu waibuka kilimanjaro

BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha Mabogini, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wanaishi kwa taharuki kubwa kutokana na taarifa za kuibuka ugonjwa wa kutapika damu unaodaiwa kuua watu watano hadi sasa.
Hadi sasa, zaidi ya wakazi 10 waishio kijijini hapo wanasumbuliwa na ugonjwa huo licha ya kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali mkoani humo ikiwemo KCMC iliyopo Mjini Moshi.
Kutokana na taharuki hiyo, Majira lilifika kijijini hapo, kuzungumza na baadhi ya wagonjwa akiwemo, Sangiwa Muro, Musa Ibrahim na Neema Joel ambao walidai dalili kuu za ugonjwa huo ni maumivu makali ya kichwa, tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kupoteza fahamu.
Kwa upande wake, Muro alisema alianza kuugua ugonjwa huo Juni, 2013 na kwenda Hospitali ya KCMC zaidi ya mara nne ili kupatiwa matibabu baada ya kutapika damu na kupoteza fahamu. Akizungumza kwa niaba yake, mama yake mzazi Bi.Fatina Abdalah, alisema mwanaye (Muro), alilazwa hospitalini hapo siku sita, kutoka Mei 14 mwaka huu, baada ya kudondoka, kupoteza fahamu na alipoamka, alianza kutapika damu.
“Ugonjwa huu umesababisha familia yetu tuishi katika mazingira magumu... kila ninapompeleka mwanangu hospitali, tunatumia fedha nyingi za matibabu hasa kwenye dripu bado kulipia dawa, vipimo, chakula, kitanda, usafiri wa kwenda na kurudi hospitali,” alisema.
Naye Joel alisema, alianza kutapika damu kuanzia mwaka 2000 wakati akifanya kazi kwenye shamba la Chuo cha Mafunzo ya Kilimo Kilimanjaro (KATC) lakini aliacha baada ya kuugua.
Alisema kila mwaka inapofikia Juni hadi Agosti, anakumbwa na ugonjwa huo na kusababisha ashindwe kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali akitumia gharama kubwa kupata matibabu.
“Huwa nikilazwa KCMC, natumia wastani wa sh 500,000 hadi 600,000, huwa siponi bali napata nafuu na kurejea nyumbani... matibabu ya ugonjwa huu ni ghali hivyo tunaiomba serikali itusaidie kufanya utafiti wa kina ili kubaini chanzo chake katika kijiji chetu,” alisema.
Mtendaji wa kijiji hicho, Hamad Mdimu alidai kutokuwa na taarifa za ugonjwa huo lakini Mwenyekiti wa kijiji, Nuhu Mnango, alithibitisha kuwa ugonjwa huo upo na wagonjwa wapo.
“Ni kweli kuna watu wanaugua ugonjwa huu hapa kijijini lakini si wa mlipuko...kati ya wagonjwa waliopo nawafahamu watatu au wanne,” alisema Mnango.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Moshi Vijijini, Timoth Wonanji, alidai kutofahamu uwepo wa ugonjwa huo lakini aliahidi kufuatilia ili kupata taarifa za kina. Hata hivyo, Daktari Bingwa Kitengo cha Upasuaji na Magonjwa ya Njia ya Mkojo katika Hospitali ya KCMC, Dkt. Mark Mvungi, alikiri kupata taarifa za wagonjwa wanaougua ugonjwa huo kutoka Kata ya Mabogini.
“Ugonjwa huu husababishwa na kupasuka, kujeruhika kwa mishipa ya damu katika mfumo wa chakula, uvimbe katika mfuko wa chakula, vidonda vya tumbo vinavyosababisha kuvuja damu na kuingia katika mfuko wa chakula.
Dkt. Mvungi alisema, sababu nyingine ni mwili kushambuliwa na magonjwa kama kichocho na vidonda vya tumbo lakini ulevi wa kupindukia hususani wa pombe kali za kienyeji ikiwamo gongo.
“Kitendo cha baadhi ya watu hasa wakulima wa zao la mpunga kutotumia viatu maalumu wakati wa kuandaa mashamba husababisha wapate ugonjwa wa kichocho kwa kuingiliwa na konokono wanaoeneza ugonjwa huu.
“KCMC ni Hospitali ya Rufaa, hapa tunapokea wastani wa wagonjwa watatu hadi wanne kwa mwezi wenye ugonjwa huu, wengi wao wanajirudia karibu kila mwaka,” alisema.

article-0-06DC6B4400000514-752_634x549
Eden Hazard amedai kuwa kwa `asilimia 100` atabakia Chelsea na amethibitisha kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.
 Kocha wa Paris Saint Germain, Laurent Blanc alisema hadharani kuwa klabu hiyo ya Ufaransa inatamani kumsajili mshambuliaji huyo.
Lakini mtandao wa Sportmail alhamisi iliyopita ulitoa taarifa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji yuko katika harakati za kusaini mkataba mpya wa miaka mitano katika klabu yake ya Chelsea na atakuwa analipwa paundi laki mbili kwa wiki.
Committed: Eden Hazard insists he is happy to remain at Chelsea, ending speculation about a summer transfer
Kujifunga: Eden Hazar amesisiza kuwa na furaha kubakia Chelsea na kumaliza tetezi za uhamisho majira ya kiangazi.
Focus mode: Hazard is currently preparing to represent Belgium in the 2014 World Cup in Brazil
 Hazard kwasasa anajiandaa kuiwakilisha Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil.

 ‘Nibakia Chelsea, nina asilimia 100`, alisema nyota huyo mwenye miaka 23.
`Kiukweli katika mpira huwezi kujua, lakini nipo chini ya mkataba na Chelsea na nataka kukaa pale`.
“Nipo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Chelsea. Mazungumzo ndio kwanza yanaanza, lakini bado tuna muda”.
“Lakini ukweli ni kwamba, Chelsea wamenipa ofa ya mkataba mpya ambao utanifanya nijiamini zaidi, kwamba nitafanya kazi nzuri zaidi na watanifurahia”
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=1844#sthash.XMC2Hm4o.dpuf

No comments: