Saturday 14 June 2014

Uholanzi waifundisha uhispania soka kwa kuichapa 5-1

 Moja ya mechi za kuvutia na yenye ushindani mkubwa ilichezwa leo katika fainali za kombe la dunia hatua ya makundi baina ya mabingwa watetezi Hispania na Uholanzi.

Uholanzi walifanikiwa kuwafunga bila huruma wapinzani wao hao kwa jumla ya goli 5-1. Hispania ndio walikua wa kwanza kupata goli kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Xabi Alonso baada ya Diego Costa kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Mvua ya magoli iliwageukia Hispania kwa kupokea kichapo hiko kwa magoli ya Robin Van Persie, na Roben wote wakitia kimyani mawili mawili. Na goli jingine moja kufungwa na Stefan De Vrij.
Uholanzi wameishangaza dunia kwa kuwafunga mabingwa hao watetezi idadi hiyo ya magoli. Uholanzi walitolewa na Hispania katika hatua ya nusu fainali ya mashindano haya hapo 2010

No comments: