Sunday 1 June 2014

Ukraine yamtangaza Poroshenko mshindi wa uchaguzi wa rais

Tume ya uchaguzi ya Ukraine imemtangaza mfanyabiashara Bw Petro Poroshenko kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo baada ya kupata asilimia 54.7 ya kura zilizohesabiwa. Bw Poroshenko anatarajiwa kuapishwa rasmi kati ya Juni 8 na 10 mwaka huu. Bw Poroshenko mwenye umri wa miaka 48 aliwabwaga wapinzani wake wa karibu Bibi Yulia Tymoshenko ambaye alipata asilimia 12.82 na Bw Ole Lyashko aliyepata asilimia 8.32 kwenye uchaguzi huo uliofanyika Mei 25. Bw Poroshenko aliahidi kuuza biashara zake zote na kumaliza msukosuko wa kisiasa pindi atakapochaguliwa rais wa nchi hiyo. Bw Poroshenko pia ameahidi kuandaa uchaguzi wa bunge kabla ya mwaka huu kumalizika. Zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura milioni 35.5 walijitokeza kwenye uchaguzi huo ambao umefanyika miezi mitatu tu baada ya Bw Victor Yanukovych kuondolewa madarakani na kukimbilia nchini Russia

No comments: