Saturday 7 June 2014

UN kumwanzi Nelson mandela

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limeridhia kuanzishwa kwa tuzo ya Nelson Mandela kutokana na msimamo wake katika kusaka haki na usawa kwa wote. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.
Hayati Nelson Mandela akihutubia Baraza Kuu la UM enzi za uhai wake.
.
(Taarifa ya Priscilla)
Ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu Ban Ki-Moon punde baada Rais wa Baraza Kuu John Ashe kutangaza kupitishwa kwa azimio namba A/68/L48 kuhusu tuzo ya Nelson Mandela. Tuzo hiyo inalenga kuendeleza kazi aliyotetea Mandela ya usawa wa binadamu na haki zao kwa kuwatia moyo wale wanaosimamia misingi hiyo ambayo pia Umoja wa Mataifa unazingatia.
Bwana Ban amesema kitendo cha leo ni hatua nyingine zaidi ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha kile ambacho Hayati Mzee Mandela aliamini na hivyo ni vyema kuendeleza kwani…
(Sauti ya Ban)
Kama alivyofahamu Nelson Mandela, mapambano bado yanaendelea. Bado kuna ubaguzi mkubwa duniani, ukosefu wa usawa , chuki baina ya watu na jamii zimegawanyika na mataifa yanapigana. Shukrani yetu kubwa kwa Mandela si katika maneno au shereha, bali ni vitendo vya kukimbiza mwenge aliotuachia."
Mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Kingsley Mamabolo akatoa shukrani..
(Sauti ya Kingsley)
"Kwa kuridhia azimio kuhusu tuzo ya Mandela Umoja wa Mataifa umedhihirisha shukrani zake kwa dhima ongozi ya Mandela kwenye harakati za ukombozi wa Afrika na Umoja wa Afrika."
Katika hatua nyingine Baraza Kuu limejadili ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu utekelezaji wa maazimio ya kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi likieleza maendeleo yaliyopatikana katika kudhibiti ugonjwa huo.

No comments: