Thursday 24 July 2014

Ndege ya Algeria yapotea na watu 116

Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116
Shirika la ndege la Algeria , Air Algerie, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake ilipokuwa ikitoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.
Afisa huyo anasema kuwa ndege hiyoya Air Algerie ilikuwa imepaa dakika 50 katika anga ya Sahara mara ya mwisho mawasiliano yao.
Ndege hiyo iliokuwa inaeelekea mji mkuu wa Algiers, ilikuwa na watu mia na kumi na wahudumu sita .
Oparesheni ya dharura ya kuitafuta ndege hiyo ieanzishwa,
Ndege hiyo nambari AH 5017 inamilikiwa na shirika la ndege la kihispania la Swiftair.
Mwandishi wa Ukomboz aliyeko katika mji mkuu wa Mali Bamako anasema kuwa kuna habari kuwa ndege hiyo huenda ilianguka katika eneo la janga la sahara kati ya
mji wa Gao and Tessalit .
Mwandishi huyo wa ananukuu ripoti kutoka kwa wanajeshi wa kulinda amani walioko huko Mali na duru za shirika la habari la AFP.
Brigadia mkuu wa majeshi ya kulinda amani nchini Mali Koko Essien, amesema kuwa maeneo hayo ya jangwani yana idadi ndogo sana ya wakaazi kwa hivyo ni vigumu kupata habari kutoka huko na inawabidi kutafuta ilikoanguka ndege hiyo.
Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116
Aidha Brig Essien anasema kuwa eneo hilo linamilikiwa na wapiganaji waasi .
Wamiliki wa ndege hiyo Swiftair wamesema kuwa ndege hiyo aina ya MD83 ilikuwa imeomba kubadili uelekeo wake kutokana na hali mbaya ya anga na ukungu mkubwa karibu na mpaka wa Algiers.
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP imeripoti.
Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.
Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo.
Tukio hili la hivi punde Linaloongeza wasiwasi kuwa njia inayotumiwa na misafara ya ndege ziendazo sehemu hiyo inapitia eneo lenye utata la anga ya Mali.

No comments: