Monday 14 July 2014

Ujerumani wanyakua Kombe la Dunia

Ujerumani ndio mabingwa wa kombe la dunia Brazil 2014
Mario Götze anaipatia Ujerumani bao la ushindi.
Ujerumani wanakuwa timu ya kwanza ya kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika mchuano ulioandaliwa Kusini mwa Marekani.
Ujerumani ilihitaji bao la muda wa ziada la Mario Gotze kuinyamazisha Argentina katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Maracana.
Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.
Kipa Nuer wa Ujerumani alituzwa ''Golden Glover'' Huku Messi akituzwa kama mchezaji bora 'Golden Ball''
Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''.
Ijapokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo la ''Golden Ball''.
Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.
Rais wa Urusi Vlamir Putin alipokea ithibati rasmi ya kuandaa makala yajayo ya kombe la dunia kutoka kwa rais wa FIFA na rais wa Brazil.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwepo Maracana kwa mualiko wa rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Brazil Dilma Rousseff.
Putin alipewa ithibati rasmi ya kuwa mwenyeji wa makala yajayo ya kombe la dunia la mwaka wa 2018.

No comments: