Tuesday 22 July 2014

UNRWA yasambaza misaada kutoka Dubai kwa wakimbizi 100,000 wa Palestina

Mtoto huyu wa kipalestina asimama nje ya nyumba iliokuwa nyumba yao iliyoharibiwa baada ya mashambulizi ya angani kambini mji wa Rafhakusini mwa Ukanda wa Gaza

Wakati raia wanaotafuta hifadhi katika kambi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA, wanatarajiwa kufika 100,000, mashirika ya kibinadamu yameshirikiana ili kusambaza misaada kutoka Dubai kwa njia ya ndege. Taarifa zaidi na John Ronoh.
(Taarifa ya Ronoh)
Kituo cha Kibinadamu cha Kimataifa (IHC), kilichopo Dubai, ni Shirika lisilo la kiserikali linaloratibu ukusanyaji, usafiri na usambazaji wa misaada ya kibinadamu.
Shirika hilo limekusanya michango ya serikali ya Falme za Kiarabu UAE, na ya mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yakiwemo lile la wakimbizi UNHCR, la Kuhudumia Watoto UNICEF, na la Mpango wa Chakula Duniani WFP kwa kipindi cha masaa 24 na limefanikiwa kupeleka shehena kubwa ya vifaa leo tarehe 21, Julai, kwa njia ya ndege. Msaada huo ni pamoja na magodoro 45,000, blanketi 10,000 na vifaa vya kujisafi kwa ajili ya wakimbizi wa Gaza.
Mkurugenzi wa UNRWA, Pierre Krahenbuhl amesema huo ni mfano bora wa ushirikiano kati ya mashirika ya kibinadamu.
Wakati huo huo, Baraza la Haki za Binadamu limetangaza kuitisha mkutano maalum kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Palestine yaliyokaliwa. Mkutano huo utafanyika, jumatano, tarehe 23, Julai mjini Geneva.

No comments: