Saturday 19 July 2014

Wapatanishi wataka mazungumzo Sudan Kusini

Wapatanishi wataka mazungumzo Sudan Kusini Viongozi wa kieneo wanaosimamia upatanishi wa mgogoro wa Sudan Kusini, wamezitaka pande hasimu nchini humo kufanya mazungumzo haraka kwa lengo la kuikwamua nchi hiyo na mzozo wa ndani. Aidha viongozi hao wameonya kuwa, ikiwa mazungumzo hayo hayatafanikiwa, basi nchi hiyo changa zaidi barani Afrika, itarajie kukumbwa na matokeo mabaya. Hayo ni kwa mujibu wa matamshi ya jana ya Hailemariam Desalegn, Waziri Mkuu wa Ethiopia aliyeongeza kuwa, kila mazungumzo huwa yana ukomo na ni lazima yafikie mwisho. Desalegn ameisitiza kuwa, nchi za eneo hilo hazipo tayari kuona mazungumzo ya Sudan Kusini yakiendelea bila natija huku raia wa nchi hiyo wakizidi kuteseka. Amezitaka pande hasimu kuwafikiria kwanza wananchi wao badala ya kulinda maslahi yao binafsi. Amesema kuwa, nchi za eneo hilo zinatoa tena fursa kwa mahasimu wa Sudan Kusini kuhakikisha wanaelewana, na ikiwa hayo hayatafikiwa basi nchi hizo hazitakuwa tayari kunyamanzia mauaji dhidi ya raia.

No comments: