Monday 1 September 2014

Liverpool yaibamiza Totenham 3-0

Wachezaji Liverpool wakishangilia ushindi
Katika mechi ya kwanza Meneja wa Liverpool Brenden Rodgers alitimiza mechi yake 100 tangu aichukue usukani wa kuifundisha liverpool kwa kushuhudia timu yake ikiisambaratisha Tottenham Hotspur kwa jumla ya magoli 3 kwa 0.

Baadae Nahodha wa timu hiyo Steven Gerrald katika dakika 49 akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penalty baada ya Joe Alllen kudondoshwa kwenye kisanduku cha 18 kwenye goli la Tottenham.Liverpool walianza kuonja ushindi katika dakika ya 8 kwa goli lililofungwa na Raheem Sterling.
Goli la tatu la Liverpool lilifungwa na Alberto Moreno Perez baada ya kuwatoka mabeki wa Tottenham na kufunga goli la tatu katika dakika 60.
Hadi mechi hiyo inamalizika Tottenham 0 Liverpool 3
Nayo Aston Villa ambao waliiadhibu Hull City magoli 2 na Hull City 1.
Aston Villa ndio walioanza kufunga goli lililofungw Gabriel Agbonlahor katika dakika ya 14.
Aston villa wakaandika goli la pili ambalo lilifungwa na Andreas Weimann katika dakika ya 36.
Nao Hull City walipata goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Nikica Jelavic.
Mechi ya mwisho iliyomalizika usiku ilikuwa ni kati ya Leicester City na Arsenal na matokeo ni kwamba Leicester goli 1 na Arsenal wamepata goli 1.

Kwa matokeo hayo sasa Chelsea ndio wanaoongoza msimamo wa ligi ya England kwa pointi 9 wakifuatiwa na Swansea iliyoshika nafasi ya pili nayo ikiwa na pointi 9 ila ikiwa na toufuti ya magoli Aston Villa ya tatu, Manchester City ya nne, Liverpool ya tano, Tottenham ya sita, Arsenal ya saba na Manchester United ikishika nafasi ya kumi na nne.

Kocha wa simba ampa Maximo Ushauri



juma kaseja 
MARCIO Maximo amefunga mjadala kwa kutamka kwamba Deo Munishi ndiye kipa namba moja wa Yanga, lakini kocha wa makipa wa Simba, Idd Pazi amesema kuwa kati ya makipa wote Tanzania anayestahili kuwa namba moja ni Juma Kaseja.
Pazi alisema kuwa katika nafasi hizo kunakuwa na makipa wa aina mbili, kipa mwenye kipaji na kipa wa mazoezi huku akimtaja Kaseja kuwa ni kipa mwenye kipaji.
Alisema kuwa mbali na kuwa na kipaji, lakini Kaseja ni kipa anayejituma bila kukata tamaa japo amekuwa akipewa tuhuma mbalimbali kutoka kwa mashabiki.
“Sijawahi kuona kipa mzuri kama Kaseja, kwanza ana kipaji, anajitambua na hata ukikutana naye mara nyingi mazungumzo yake ni soka na maendeleo yake katika hilo, ni kipa ambaye yupo wazi kutaka kujua jambo litakalomsaidia,” alisema.
“Makipa Tanzania wapo wengi, lakini wengi wao ni makipa wa mazoezi kwamba afanye sana mazoezi ndipo alinde kipaji chake.
“Lakini hiyo ni tofauti kabisa kwa Kaseja, nimemfundisha na hata sasa hivi huwa anahitaji kufundishwa pale anapokuwa na muda wa ziada, hivyo unaona kabisa kwamba huyu ni kipa mwenye malengo.
“Ndiyo maana ninasema Kaseja ndiye namba moja nchini.”
Alisema kuwa wengi wanadai umri wa Kaseja umekuwa mkubwa ndiyo maana kiwango chake kimeshuka, lakini yeye alisistiza kuwa kipa huyo ana miaka zaidi ya miwili katika soka.
“Hapa Simba kuna huyu kijana Manyika Peter, kama hatalewa sifa na akajitambua naye atafika mbali kama Kaseja,” alisema Pazi.

Kocha wa simba ashangazwa na usajili wa Okwi



phiri
USAJILI wa straika Emmanuel Okwi ndani ya Simba, umemshtua kocha Patrick Phiri ambaye amesema haelewi nini kimetokea na sasa amewaachia viongozi waamue nani anafaa kuachwa ama kuendelea.
Juzi Alhamis jioni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe, alimtangaza rasmi Okwi kuwa mchezaji mpya wa Simba kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mpaka jana Ijumaa mchana Okwi alikuwa hajajiunga na kambi hiyo iliyopo visiwani hapa huku kukiwepo taarifa kuwa angewasili muda wowote na taarifa za ndani zilisema kuwa beki Mkenya Donald Mosoti ndiye aliyekuwa kwenye mpango wa kuachwa.
Simba ilipitisha majina ya wachezaji 28 wakiwemo wachezaji watano wa kigeni ambao ni washambuliaji Amissi Tambwe, Raphael Kiongera, Pierre Kwizera, Joseph Owino na Mosoti.
“Bado nipo gizani, nimesikia taarifa hizo lakini nasubiri taarifa ya viongozi, naamini uongozi wa Simba upo vizuri katika kusajili hivyo mchezaji nitakayeletewa atakuwa mzuri maana wao wamemuona na amewahi kuichezea Simba,” alisema Phiri.
“Soka la Tanzania ni kama siasa hivyo tunatakiwa kukubaliana na hali halisi, mimi ni mtaalamu wa benchi la ufundi lakini viongozi pia wana utaalamu wao, hivyo naamini usajili wao utakuwa mzuri.”
Kuhusu taarifa za kutemwa kati ya wachezaji wake Mosoti au Tambwe, Phiri alisema: “Mosoti sikumpa nafasi sana ya kucheza mechi hizo kwa sababu wengi wanamfahamu na Butoyi Hussein amekuja kwa ajili ya majaribio hivyo ilikuwa ni lazima apewe nafasi ili aonyeshe kiwango chake.
“Tambwe ni mchezaji mzuri na ndiye mfungaji bora wa ligi msimu uliopita, binafsi alicheza vizuri pamoja na Said Ndemla katika mechi zilizopita, nikiwa kama kocha siwezi kusema mchezaji ameshuka kiwango kwa mechi za kirafiki.”

Kwezera ashangaa wing wa mashabiki wa simba



KIUNGO wa Simba, Mrundi Pierre Kwizera amesema hajawahi kucheza timu yenye wingi wa mashabiki kama klabu hiyo ya Msimbazi na ndiyo wanamshawishi ajitume na kufanya kazi kwa bidii ili kuwapa kile wanachokitaka.
Kwizera amesajiliwa na Simba msimu huu, akitokea nchini Ivory Coast alikokuwa anakipiga klabu ya Afad Abdijan.
Ameliambia ukomboz akisema: “Sijawahi kucheza kwenye klabu yenye mashabiki wanaopenda timu yao kama Simba, nimependa sana.
“Mashabiki hawa wananipa raha na ndiyo wanaonishawishi nifanye kazi yangu kwa ustadi na nguvu ili niwaridhishe kwa kuwapa kile kitu wanachopenda.”
Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Burundi anayevaa jezi namba nane, amekuwa akifanya vizuri kwenye mechi za kirafiki alizocheza pamoja na mazoezini na kuwashawishi mashabiki wamkubali.
Beki wa kikosi hicho cha Msimbazi, Nassor Masoud ‘Chollo’ ametamka kuwa mchezaji atakayeshindwa kuishi na kufanya kazi na kocha wao mkuu wa sasa, Mzambia Patrick Phiri atakuwa na matatizo makubwa.
Chollo anafanya kazi na Phiri kwa mara nyingine baada ya kumfundisha hapo awali na kumwelezea, huwa hana matatizo na mchezaji yeyote kama utamsikiliza na kumfuata anachokitaka.
Chollo aliambia ukombozi “Makocha wengine huwa na matatizo lakini kwa huyu Phiri utakuwa unamwonea, tena kwa mchezaji yeyote anayeshindwa kufanya naye kazi, atakuwa na matatizo binafsi.”
“Nimekaa na makocha wengi, lakini kwa huyu jamaa ni sawa na mzazi kwa kila mchezaji, anakuelekeza na unapokosea anakaa na wewe kama mzazi mnayaweka sawa, hadi mtofautiane, lazima mchezaji husika atakuwa na matatizo.”