Wednesday 29 October 2014

Cabaye atamani kucheza pamoja na Hazard

KIUNGO wa PSG, Yohan Cabaye amesema anapenda kuona siku moja mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard anaichezea timu hiyo kwani ni kati ya wachezaji anaowakubali kwa kiasi kikubwa. Mchezaji huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Ufaransa, alisema anamfahamu vizuri Hazard kuwa ni kati ya wachezaji wazuri mno ambapo kama atafanikiwa kujiunga na timu yake ataweza kuongeza ushirikiano kwa kiasi kikubwa. Alisema, anatarajia kufanya mchakato wa kushawishi uongozi wake ili kuhakikisha anatua PSG. "Hazard ni mchezaji mzuri ambaye nitafurahi zaidi kumwona anaitumikia PSG, kwani ni kati ya wachezaji ninaowafahamu vizuri. "Ni mchezaji wa kuangaliwa kwa kiasi kikubwa kwani anatumia akili nyingi kucheza mpira na hufanya vizuri kila wakati," alisema.

No comments: