Saturday 25 October 2014

Filipe Nyusi rais mpya wa Msumbiji

Tume ya Uchaguzi Msumbiji: Nyusi mshindi wa UraisFilipe Nyusi mgombea wa kiti cha urais nchini Msumbiji ametangazwa na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuwa mshindi wa kiti cha Urais baada ya kura zote kuhesabiwa.
Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 15 yaliyotangazwa leo na Tume ya Uchaguzi ya Msumbiji yanaonesha kuwa, Filipe Nyusi mgombea wa chama tawala cha Frelimo amepata asilimia 57 ya kura. Mgombea wa chama cha upinzani cha Renamo, Afonso Dhlakama amepata asilimia 36 ya kura huku Davidz Simango wa chama cha Mozambique Democratic Movement akiambulia karibu asilimia 7 tu ya kura.
Kwa mujibu wa katiba ya Msumbiji, matokeo hayo yanapaswa kupasishwa na Mahakama ya Katiba kabla ya kuwa rasmi. Chama cha Frelimo ambacho kimekuwa kikiiongoza Msumbuji tangu mwaka 1975 pia kimedhibiti Bunge baada ya kupata wingi wa viti katika Bunge la nchi hiyo lenye viti 250.
Renamo ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kimepinga matokeo hayo na kusisitiza kwamba, uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na wizi wa kura. Hata hivyo waangalizi wa kimataifa wametangaza kuwa, uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira huru na ya haki.

No comments: