Friday 24 October 2014

UKAWA waapa kwenda mahakamani kupinga Katiba kupigiwa kura

MUUNGANO wa Vyama Vya Siasa nchini vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA ), wanatarajia kufungua kesi mahakamani ili kuzuia mchakato wa kura ya maoni ya Katibainayopendekezwa uliopangwa kufanyika Aprili 2015,

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba aliyasema hayo juzi wakati akihojiwa na Sauti ya Amerika (VoA),akisema chama chake kimeshiriki kuandaa mashtaka hayo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),Jaji Fredrick Werema, kutangaza kuwa mchakato wa kura za maoni kwa Katiba Mpya utafanyika mwakani .
Katika mahojiano hayo,Prof.Lipumba, ambaye aligombea urais kupitia chama chake mwaka 2010, alisema uongozi wa Rais Jakaya Kikwete umeshindwa kufuata sheria wakati wakupitisha Rasimu inayopendekezwa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba hatua ambayo inaweza kuleta machafuko nchini.
“Katiba iliyopendekezwa haikupitishwa kisheria kwenye Bunge la Katiba, kulikuwa na kura za Zanzibar na Tanzania Bara lakini chakushangaza,Rasimu imepitishwa wakati Zanzibar haikuwa na kura za kutosha kufikia theluthi mbili ya wajumbe,” alisema .
Prof.Lipumba alisema uamuzi wa wajumbe wa Bunge hilo kutoka UKAWA kususia Bunge,ulitokana na Serikali kushindwa kuingiza mapendekezo yao yakiwemo mageuzi ya kisiasa kwenye Katiba inayopendekezwa.
“Tulisusia Bunge la Katiba kwa sababu sheria haikuheshimiwa nautaratibu ulitawaliwa na udanganyifu tangu siku ya kwanza hivyo tukaona hatuwezi kuendelea na mchakato huo;tukatokanje ili kushinikiza kilio chetu kisikilizwe,”alisema.
Aliongeza kuwa, kuna ishara kwamba muda uliobaki hadi kufikia Aprili 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),haitaweza kuwaingiza wapiga kura wapya ambao wamefikisha umri wa kupiga kura kwa ajili ya kura ya maoni ili kupitisha Katiba Pendekezwa.
“Kama NEC haina Daftari la Kudumu la Wapiga kura lililoboreshwa kwa kuandikisha wapiga kura wapya,kwanini watangaze kura ya maoni wakati hata tume haijajiandaa na uchaguzi ujao ?
“Watu wengi hawajajiandikisha, vijana wote ambao walikuwa na miaka 17 au chini ya hapo mwaka 2010, hawajaandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura, kuna watu zaidi ya milioni tano ambao bado hawajaandikishwa,” alisema Prof. Lipumba.
Aliongeza kuwa;“Umaarufu wa Serikali umeshuka,wanataka kuiba kura ili washinde na sisi tunasema hapana, hatukubaliani na udanganyifu katika uchaguzi,” alisema.
Wachambuzi wa masuala ya siasa,wanaamini Katiba Mpya nchini Tanzania huenda ikapitishwa kwenye kura ya maoni japokuwa Prof.Lipumba hakubaliani na hilo.
Kwamujibu wa VOA, baadhi ya wafuasi wa chama tawala CCM, wanasema vyama vya upinzani ndivyo vyakulaumiwa kwakususia Bunge hilo wakati wa Katiba Pendekezwa

No comments: