Friday 31 October 2014

Rais wa Burkinafaso ang'olewa madarakani


Kuna hofu kuwa rais Compaore anataka kuendelea kushikilia madaraka
Msemaji wa jeshi amewaambia waandishi wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena.
Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpwito ya mwaka mmoja .
Lakini wanasiasa wa upinzani wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja.
Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miaka 27 tayari.
Kumeripotiwa maandamano mapya nchini Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Viongozi wa upinzani wanakutana kwenye mkji mkuu Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua.
Siku ya Alhamisi waandanamaji walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27 madarakani na wakateketeza bunge na kusaka kituo cha runinga cha serikali.
Rais Compaore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa atabaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
Viongozi wa Upinzani Nchini Burkina Faso wamewaomba waandamanaji kutolegeza kamba bali kuendelea na maandamano huku wakimtaka Rais Blaise Campaore ang'atuke mamlakani mara moja.
Licha ya Rais Compaore wa Burkina Faso kuhutubia taifa siku moja baada ya vurugu kubwa na kutangaza kuvunja serikali waandamanaji hawataki kusikia kwamba apewe muda wa mwaka mmoja ndipo aondoke madarakani.
Jana jioni kiongozi wa Jeshi  General Honore Traore alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpito itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja japo hakusema ninani atakayeiongoza.

No comments: