Friday 21 November 2014

Ivory Coast inaweza kukabiliwa na vikwazo baada ya mashabiki kuvamia uwanja

Timu ya soka ya Ivory Coast huenda ikakabiliwa na vikwazo baada ya mashabiki wake kuvamia uwanja mjini Abidjan baada ya kuweza kufuzu kuiwakilishwa nchi katika michuano ya mataifa ya bara la Afrika mwakani. Tukio hilo lilitokea baada ya timu hiyo kuondoka na sare ya bila kufungana dhidi ya Cameroon siku ya Jumatano na kujihakikisha kuwa wanamaliza wakiwa nafasi ya pili katika kundi lao D. Shrikisho la soka barani Afrika CAF limesema linasubiri ripoti ya refa kuhusu tukio hilo. Tukio hilo huenda likashughulikiwa na kamati ya maandalizi mnamo Disemba mosi. Polisi walihangaika kuhakikisha wanarejesha utulivu, baada ya mashabiki kuvamia uwanja. Picha zilizochukuliwa wakati mashabiki wakivamia uwanjani zinaonesha kuwa mashabiki walitandikwa viboko na askari wa usalama, huku wengine wakijaribu kuchana kaptula ya Gervinho.

No comments: