Saturday 8 November 2014

Kocha wa Kagera Suger amtamani Jaja

Straika wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’
KOCHA mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja, amemwangalia straika wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’ kwa dakika 90 na kutamka kuwa kama angepewa mchezaji huyo, basi angemtengeneza na kumfanya kuwa mtu hatari sana mbele ya lango.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha huyo alisema Jaja ana vitu vidogo sana vya kumrekebisha na kama angekuwa ni mchezaji wake, basi angemwekea programu maalumu ambayo ingemfanya aweze kuwa straika hatari.
Mayanja alisema alimwangalia Jaja ndani ya dakika 90 za mchezo wao dhidi ya Yanga uliopigwa Jumamosi iliyopita na kugundua vitu vidogo mno vya kumrekebisha.
“Jaja ni moja ya wachezaji hatari kuwahi kuwaona kwangu, ila ningekaa naye kwa muda, ningemtengenezana watu wangemshangaa, tatizo lake la kwanza ni uzito ningemfanya awe mwepesi  na mambo mengine ya uwanjani namna ya kupambana na mabeki,”alisema Mayanja.
“Anahitaji mabeki makini kumkaba uwanjani kwanza ni mrefu anatumia umbo lake katika mipira ya vichwa ni mchezaji mzuri mno, anaweza kujipanga na kujua wapi mpira utaweza kumfikia kwa urahisi,”alisema kocha huyo raia wa Uganda.

No comments: